CURRENT NEWS

KITAIFA

Siasa

MICHEZO NA BURUDANI

Thursday, October 30, 2014

UHABA WA FEDHA KUATHIRI MECHI ZA MALAWI

Malawi imetangaza kuwa huenda ikashindwa kushiriki katika mechi za kufuzu kwa dimba la bara afrika mwaka 2015 kwa kuwa haina fedha za kucheza mechi zake mbili za mwisho.
Kufikia sasa Malawi iko katika nafasi ya tatu katika kundi Ba ikitarajiwa kucheza na Mali na Ethiopia.

Katibu mkuu wa Shrikisho la soka nchini Malawi Suzgyo Nyirenda ameiambia BBC kwamba wanajaribu kutafuta mfadhili ili kugharamia maandalizi ya mechi hizo.

Hatahivyo amesema kuwa uamuzi kamili utatolewa kati tarehe 4 na 5 mwezi Novemba.
Malawi inatarjiwa kucheza na Mali nyumbani tarehe 15 mwezi Novemba kabla ya kusafiri hadi Ethiopia siku nne baadaye.

Iwapo watashindwa kupata fedha za kusimamia mechi hizo,wataondolewa katika michuano hiyo hatua itakayoathiri nafasi yao ulimwenguni.

Malawi imepata ushindi dhidi ya Ethiopia lakini ikapoteza dhidi ya Mali.

Iwapo matokeo hayo yatatupiliwa mbali basi ,itamaanisha kwamba Ethiopia na Mali zitakuwa na alama sawa na kupigania nafasi ya pili kufuzu nyuma ya Algeria,ambao tayari wamefuzu.

Bwana Suzgyo amesema kuwa tayari serikali imewaeleza kwamba hawataweza kusimamia gharama za mechi hizo.
Timu hiyo inahitaji takriban dola 155,000 kumaliza mechi zake.

EBOLA:MUUGUZI ATISHIA KUVUNJA KARANTINI

kaci
Muuguzi aliyewekwa chini ya karantini alipowasili Marekani baada ya kuwatibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ametishia kutoka nyumbani kwake alikozuiliwa iwapo masharti ya kumzuilia hayataondolewa.

Kaci Hickox, ambaye hadi kufikia sasa amekuwa akishirikiana na maafisa wa afya wa jimbo la Maine, anasema kuwa yeye ni mzima kabisa na hana dalili zo zote za maradhi hayo.

Hali yake imemulika tofauti kubwa zilizopo kati ya idara za afya za Serikali ya Taifa na Serikali za majimbo katika kukabiliana na Ebola.
Kaci
Wanasayansi wanaoshauri Serikali kuu juu ya Ebola wanasema kuwa hakuna haya ya kutumia karantini kama hatua ya kuzuia ugonjwa huo kusambaa.


Hata hivyo maafisa wa afya wa jimbo lake la Maine wametishia kwenda mahakamani kupata idhini ya kuwatumia wanajeshi kuhakikisha haondoki nyumbani kwake iwapo atatisha kufanya hivyo.

TANZANIA, KENYA, NA UGANDA ZANG'ARA KITEKNOLOJIA


Wakati mkutano kuhusu mipango thabiti ihusuyo teknolojia ukiendelea nchini Korea Kusini Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, shirika la wanawake UN Women  ni miongoni mwa taasisi zilizopewa tuzo za kutambua mchango wa kuendeleza maisha ya wanawake kupitia teknolojia.

Mkutano huo unaoratibiwa na Shirika la kimataifa la mawasiliano ITU pia umeshuhudia nchi za Afrika kama Nigeria zikipata tuzo lakini kubwa zaidi zile za Afrika Mashariki zimeandika historia kwa kuingia   katika baraza la utawala la ITU kwa mara ya kwanza.

Katika mahojiano na idhaa hii kutoka Korea Kusini mkuu wa mawsiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungi anadadavua vyema siri ya mafanikio hayo hususani ni kwa nchi yake na pia kueleza mambo mengine muhimu yanayojadiliwa katika mkutano huo. Kwanza anaanza kwa kueleza kuhusu utolewaji wa tuzo.

MAGAZETI YA LEO OKTOBA 30 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania